Thursday, January 21, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Amos Makalla amefanya ziara wilaya ya Rombo kwa kuweka jiwe la msingi mradi wa Maji Ngareni na kuzindua hosteli ya wasichana sekondari ya Horombo
Aidha amefanya kikao cha pamoja madiwani, watendaji wa kata na Vijiji na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama Rombo na kuelekeza yafuatayo
1. Amepiga marufuku unywaji wa pombe kupindukia, unywaji pombe wakati wa kazi na utengenezaji pombe haramu ikiwemo gongo na nyingine
2. Ameagiza Kamati ya Ulinzi kuimarisha ulinzi na msako kwa wahalifu wakiwemo majambazi toka nchi jirani ya kenya na pia wadhibiti wahamiaji haramu wanaopitia mpaka wa Tanzania













0 comments:

Post a Comment