Wednesday, January 27, 2016




MADIWANI na watumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano, badala ya `kupiga majungu.

Ushauri huo umetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Chande Nalicho wakati akitoa salamu za serikali katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani ambacho kilipitia taarifa mbalimbali za utekelezaji wa maagizo na ya serikali kuu, serikali za mitaa na utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo.

Alisema madiwani na watumishi wanapaswa kushirikiana kwa lengo la kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi, ili waweze kufaidi mipango mizuri ya maendeleo iliyopo katika mipango ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Alisema kwa kuwa uchaguzi umeshapita na viongozi wa halmashauri wameshapatikana, hakuna ulazima wa kuendeleza visa au kinyongo miongoni mwa madiwani na watumishi, bali kuanza kuwatumikia wananchi kwa kasi.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ali Mpenye ameziagiza kamati za maendeleo za vijiji, mitaa na kata kuhakikisha zinasimamia vyema fedha.

0 comments:

Post a Comment