Wednesday, January 27, 2016




MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za maofisa wanaofanya kazi kinyume na maadili.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo alisema TRA ina idara maalumu ijulikanayo kama Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA ambayo inashughulika na kufuatilia maadili ya watumishi wa sekta hiyo nchi nzima.

“Tunawaomba wananchi kushirikiana na Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA kwa kuwapa taarifa juu ya maofisa wa TRA wanaokwenda kinyume na Maadili ya Utumishi wa Umma,” alisema Kayombo.
Aliongeza kuwa, wananchi wanaweza kutoa taarifa kwa kupiga simu kwa namba 0689 122 515 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwa simu namba 0689 122 516 na kuwahakikishia kuwa taarifa zao zitakuwa zimefika sehemu husika na zitafanyiwa kazi.

Aidha, amewatoa hofu wananchi kuwa namba hizo ni za siri na hakuna mwananchi atakayepata tatizo lolote kwa kutoa taarifa za maofisa wasio na maadili.

Alisema kupitia idara hiyo, TRA imepokea malalamiko mengi na kuyafanyia kazi na kuongeza kuwa, tayari baadhi ya watumishi wamefukuzwa kazi na wengine kupewa adhabu kali.

0 comments:

Post a Comment