Jeshi
la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwanasa
wafanyabiashara wakongwe wa dawa za kulevya nchini ambao pia wanadaiwa
kufanya biashara haramu za binadamu ambao wamekuwa wakiwasafirisha
kutoka nchini kwenda katika nchi zinazozalisha dawa za kulevya.
Magwiji hao wa dawa za kulevya nchini waliotiwa nguvuni na jeshi la
polisi ni pamoja na Mohamed Abdallah Omary, Nassoro Suleiman na meneja
wa duka la Tungwe Bureau de Change ambalo hutumika kusafirisha fedha za
dawa za kulevya kwenda nchini Pakstani kinyume na sheria.
Taarifa hiyo kamanda Sirro, amesema kwasasa jeshi la polisi
limejipanga kuhakikisha linadhibiti mianya yote ya dawa za kulevya
ambapo pia katika msako mkali uliofanyika mwishoni mwa wiki gari zenye
namba za usajili T271 DCT, T916 DCL, T593 CEL na T999 DDB zimekamatwa.
Kamanda Sirro amesema kuwa kumeibuka wimbi la wafanyabiashara wa
dawa za kulevya kusafirisha watanzania kuwapeleka nchini Pakstani na
kuwaacha kama bondi ili wapatiwe mzigo mkubwa wa dawa za kulevya ambapo
wengi wao wamekuwa wakiuawa ambapo amesema jeshi limejipanga
kusambaratisha mtandao huo.
0 comments:
Post a Comment