Kundi la mawakili, wanaharakati na
wanasayansi nchini Brazil limewasilisha ombi mahakama ya juu nchini humo
likitaka wanawake wenye virusi vya Zika waruhusiwe kutoa mimba.
Virusi vya Zika vinaaminika kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo, na kudumaza ubongo.
Utoaji
mimba nchini Brazil hauruhusiwi kisheria, ila tu wakati wa dharura ya
kiafya au iwapo mimba imetokana na ubakaji hali ambayo kwa Kiingereza
inajulikana kama microcephaly.
Hata hivyo mwaka 2012, uliruhusiwa kwa watu walioathiriwa na ugonjwa mwingine wa ubongo kwa jina anencephaly.
Wataalamu
wameonya kwamba idadi ya watu walioambukizwa na virusi vya Zika mwaka
huu huenda ikafikia kati ya milioni tatu au nne mwaka huu mabara ya
Amerika.
Ombi hilo mpya litawasilishwa mahakama ya juu katika kipindi cha miezi miwili.
Kundi linaloandaa ombi hilo ndilo lililowasilisha ombi kwa niaba ya
waathiriwa wa anencephaly mwaka 2012 mahakama ya juu na kupata ushindi.
Hayo
yakijiri, Thomas Bach, mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki amesema
hatua zinachukuliwa kulinda michezo ya mwaka huu ambayo itaandaliwa
mjini Rio de Janeiro.
IOC itatoa mwongozo baadaye Ijumaa kwa wanariadha na wageni ambao wanapanga kushiriki au kuhudhuria michezo hiyo.
Brazil ndilo taifa lililoathirika zaidi na mlipuko wa Zika.
Kuna visa 270 vya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo ambavyo vimethibitishwa, kwa mujibu wa wizara ya afya nchini humo.
Kuna visa vingine 3,448 vya microcephaly ambavyo vinachunguzwa.

0 comments:
Post a Comment