Posted by Williammalecela.com on Friday, January 01, 2016
Meneja wa staa wa muziki wa Bongo Fleva
Diamond Platnumz ambaye amekuwa akiachia kazi zenye ubora unaostahili
tangu alipo ingia kwenye ramani ya muziki wa bongo fleva amesema siri nyingine ya Diamond Platnumz kufanya video kali licha ya kuwa anafanya kazi na ma ‘Director’ wa nje ya Tanzania.
Meneja wa Diamond ambaye ni Hamisi Tale
A.K.A Babu Tale amesema Diamond ni mtu ambaye anapenda vitu vizuri na
hivyo anapofikiria kufanya jambo lake huwa anatenga bajeti mara mbili ya
kitu anachotaka kukifanya.
“Kwa
mfano Diamond unapo mwambia hiki kitu ni laki moja, halafu kizuri zaidi
yake ni laki tatu huwa hasiti kutoa ili apate chenye ubora wa juu kwa
kuwa muda wote huwa anawa wazia mashabiki zake kuwapa vitu vizuri…”
alisema Tale
Licha ya Diamond kuwa na tabia ya
kutenga bajeti ya juu kwenye kazi zake, Meneja Tale alinogesha kuwa kuna
wakati Diamond hapokei video ambayo hajarizika nayo licha menejimenti
nzima kuikubali.
Babu Tale aliitolea mfano video ya “NITAMPATA WAPI” ambapo alisema mpaka kufikia hatua ya kuachiwa ilifanyiwa marekebisho kwa kurudiwa
kuhaririwa nzima nzima mara tatu na mara ya nne ndipo ilipo achiwa
rasmi, lakini pia hata video ya “UTANIPENDA”
mpaka kukamilika mhariri aliaandaa akiwa amesimamiwa na Diamond
Platnumz mwenyewe huk akiwa anamulekeza kile anachokitaka yeye kwenye
video yake.
0 comments:
Post a Comment