Friday, January 1, 2016



Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ambaye anastaafu hii leo amesema yeye ni mpenzi mkubwa wa msanii wa DRC, Koffi Olomide.
Kova amebainisha mapenzi yake kwa msanii huyo leo Jijini Dar es Salaam, alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio.

Katika kuonesha kuwa anamfuatilia kwa karibu kazi za msanii Koffi Olomide, Kamishna Kova aliomba apigiwe kibao chake kipya kinachotamba hivi sasa cha Selfie.

0 comments:

Post a Comment