Saturday, January 9, 2016

 
Mfanyabiasha mkubwa wa dawa za kulevya anaejulikana kama El Chapo amekamatwa tena, miezi mitano baada ya kukimbia kutoka  gereza lenye usalama mkali. ..,

 

Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto, alitangaza habari hizo katika ukurasa wake wa Twitter, lakini maafisa wamekataa kutoa taarifa zaidi kuhusiana na kukamatwa kwa El Chapo. Vyombo vya habari nchini Mexico vimeripoti kuwa, El Chapo Guzman, amekamatwa wakati wa mapambano ya risasi baina ya watu waliokuwa na silaha na askari wa majini wa Mexico.

 Juni mwaka jana, Guzman alitoroka jela kupitia kwenye choo cha chumba alichokuwa amefungwa na baadae kupitia bomba lenye kilomita moja na nusu hadi nje ya gereza. Hiyo ikiwa ni mara ya pili kutoroka kutoka jela, jambo lilosababisha fedheha kubwa kwa serikali ya nchi hiyo.

0 comments:

Post a Comment