Posted by Williammalecela.com on Tuesday, January 26, 2016
Same kuhusu OPERESHENI MIRUNGI SAME kimefanyika leo kwa kushikirikisha
vyombo vya Ulinzi na usalama, madiwani,watendaji wa kata na Vijiji,
wenyeviti wa Vijiji na wakuu wa vituo vya polisi Mkuu wa wilaya
ametoa taarifa kuwa siku 28 alizotoa mkuu wa Mkoa tarehe 29 dec 2015
kuwa kila Mwananchi afyeke na kungoa mirungi kwa hiari yake zimekwisha
na kwamba katika Vijiji 28, na kata 13 kati ya wakulima ya mashamba
921 yenye ekari 260 ya mirungi ni wakulima/ mashamba 313 tu Sawa na 34%
waliotekeleza agizo la mkuu wa Mkoa na Hivyo mkuu wa Mkoa Ameagiza
1. Serikali baada ya siku 5 kuanzia leo imejipanga kufanya operesheni
kabambe ya kuhakikisha mashamba yote yaliyobaki yanafyekwa na wananchi
watakaokaidi kutekekeza katika siku Tano watakamatwa na kufunguliwa
mashitaka na kwa mujibu wa sheria ya madawa ya kulevya adhabu yake ni
kifungo miaka 30 2. Ameagiza watendaji, madiwani na wakuu wa vituo vya polisi kuhamasisha wananchi kutumia siku 5 kufyeka na kungoa mirungi yote
3. Wilaya ya Same inaongoza kwa kulima, kuuza mirungi nchini ambayo
huuzwa mikoa mingi nchini na nchi jirani ya Kenya na madhara yake ni
kuathiri nguvu kazi hasa vijana, utoro mashuleni na kupelekea wilaya ya
Same kwa Matokeo ya darasa la saba kuwa na Shule sita za mwisho kimkoa
0 comments:
Post a Comment