Tuesday, January 26, 2016




Msanii wa kike anayefanya vizuri kwenye kiwanda cha muziki Tanzania, Sarah ‘Shaa’ Kaisi, amesema kuwa kufunga ndoa sio mwisho wa matatizo kama wengi wanavyodhani.

Akizungumza kuhusu mahusiano yake kupitia kipindi cha Pillow Talk cha Times Fm, Shaa amesema yeye yupo kwenye uhusiano mwaka wa 10 sasa, na haoni sababu ya kukimbilia ndoa kabla hajajiweka sawa kiuchumi. “Ndoa sio solution ya kila kitu unajua, yaani ukiolewa tu umemaliza matatizo NO, unahitaji kujiweka sawa na kujiandaa” Alisema.

Hata hivyo mwana dada huyo anaekimbiza na wimbo wake wa Toba, ameweka wazi kuwa miaka 3 ijayo anaweza akaingia ndani ya ndoa

0 comments:

Post a Comment