Mabingwa wa Tanzania Bara Timu ya
Yanga, wamefanikiwa kutinga hatua ya Nusu fainali kufuatia ushindi wa
mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa mabao ambayo yamefungwa na wachezaji Aboubakar
na Malimi Busungu na kuwa kinara wa kundi B la michuano ya Kombe la
Mapinduzi baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 7...,
Katika mchezo mwingine wa mapema wa kufuzu hatua ya nusu fainali, timu ya mafunzo imeichapa Azam FC 2-1 kwa ushindi usio na faida kwa timu hiyo baada ya kutupwa nje ya mashindano hayo kwa uchache wa pointi.
Yanga sasa watacheza nusu fainali na mshindi wa pili wa Kundi A huku Mtibwa Sugar nao wakikutana na mshindi wa kundi hilo.
Kundi A linamaliza mechi zake leo Ijumaa kwa Timu ya Jamhuri kuchuana na URA na Simba ikicheza na JKU huku kila timu ikiwa ina nafasi ya kutinga nusu fainali ikipata matokeo mazuri ingawa sare kwa Simba itawafikisha nusu fainali.
URA na Jamhuri zinahitaji ushindi.
0 comments:
Post a Comment