Dar es Salaam: Wakati mastaa wenzake Bongo, Wema Isaac Sepetu na
Kajala Masanja wakifurahia kunasa ujauzito, taarifa ambazo zimevuja
zinadai kwamba, chanzo cha Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ kumwagana na
Mwanamuziki Ali Saleh Kiba ni kufuatia kuchoropoka kwa mimba ya mrembo
huyo hivyo kumsononesha moyo wake, Ijumaa limenyetishiwa siri nzito.
Habari kutoka ‘redio mbao’ za mjini zilidai kwamba, wiki mbili
zilizopita, Jokate na Kiba waliingia kwenye gogoro zito mara tu baada ya
kuripotiwa kuchoropoka kwa ujauzito huo ikisemekana kuwa hali hiyo
ilimpata kufuatia kufanya mazoezi makali ya kudensi akijiandaa na shoo.
“Unajua
Kiba aliposikia mimba ya Jokate ambayo aliamini ni yake imechoropoka,
alihisi anafanyiwa figisufigisu na kwamba huenda Jojo hakuwa amejiandaa
kuitwa mama,” kilidai chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina na
kuongeza:
“Ndiyo chanzo cha ugomvi wa Jokate na Kiba licha ya zile sababu
nyingine za tofauti ya dini, wazazi wa Jokate kutomtaka Kiba. Bado vikao
vya kuwasuluhisha vinaendelea lakini jamaa (Kiba) anaonekana kutia
ngumu.”
Hata hivyo, habari mpya zilizolifikia gazeti hili zilidai kuwa
kumwagana kwa Jokate na Kiba kulipokelewa kwa kicheko na ndugu wa mrembo
huyo ambao tangu awali walionekana kutounga mkono penzi la wawili hao.
Gazeti hili lilipomtafuta Kiba ili kufafanua ishu hiyo, kama kawaida
simu yake iliita bila kupokelewa lakini kwa upande wake Jokate alikuwa
na haya ya kusema: “Jamani naombeni mniache, sitaki kabisa kuongelea
hayo mambo ya Ali Kiba.”
Hata hivyo, mwanahabari wetu alipotaka kusikia japo neno lake juu ya
kuachana na Kiba na kwamba chanzo ni kuchoropoka kwa ujauzito huo,
alisisitza kwamba aachwe.
0 comments:
Post a Comment