Wednesday, January 20, 2016

866e36f4c94b11e2b13b22000a9e0790_7866e36f4c94b11e2b13b22000a9e0790_7
RAPA maarufu wa wimbo wa Chocolate City, Ice Prince.
amewananga wanaotaka kumharibia mahusiano yake na mpenzi wake wa Ghana aitwaye Maima ambapo walianza kueneza uvumi mwaka jana kwamba wametengana.

Ice-Prince-Bae
Amefichua uongo huo kwa kueneza picha kibao kwenye mtandao akiwa katika pozi za mahaba na mpenzi wake huyo.“Ni ajabu watu wanataka kuniharibia uhusiano wangu na mpenzi wangu,” aliandika kwenye mtandao hivi karibuni kuhusu uvumi huo.
Maima ni mwanamke wa pili ambaye Ice Prince amekuwa na mahusiano naye ya kimapenzi. Wawili hao ambao kila mtu anaishi kivyake, kila mmoja wao ana mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili.

0 comments:

Post a Comment