Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda
Jumamosi ijayo (30.01.2016) anatarajia kuwa mgeni rasmi katika hafla ya
kusherehekea mwaka mpya wa Kichina.
Mwambata wa utamaduni katika
ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bwana Gao Wei amesema hayo
leo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu
maadhimisho ya siku ya utamaduni wa Wachina nchini.
Maadhimisho ya mwaka mpya wa
Kichina ni alama muhimu katika utamaduni wa wachina na uadhimishwa kwa
wachina kuungana pamoja na familia zao na kufanya shughuli za kitamaduni
ikiwemo michezo.
Bwana Gao Wei amaseme kuwa,
maadhimisho ya mwaka huu pamoja na kuwakutanisha jamii ya watu wa China
na viongozi mbalimbali wa serikali, yatatoa fursa za kuimarisha
ushirikiano kati ya China na Afrika, kuendeleza urafiki uliopo na
kuhakikisha kila upande unanufaika na urafiki huo.
“Serikali ya Jamhuri ya Watu wa
China pamoja na watu wake tutaendelea kujenga mazingira rafiki
kuhakikisha kila upande unafaidika na urafiki wetu,” amesema.
Bwana Gao Wei ameongeza kuwa moja
ya malengo ya maadhimisho hayo hapa nchini ni kutoa ujumbe kuwa jamii
ya Watu wenye asili ya China wanakuwa watiifu kwa serikali ya Tanzania
na kuleta usawa katika ushirikiano wa kisiasa na biashara.”
Kwa mujibu wa Mwambata huyo,
katika maadhimisho hayo yatakayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja,
Dar es Salaam, kutakuwepo na michezo mbalimbali ya utamaduni zikiwemo
nyimbo, muziki, judo, muziki wa ala, na michezo mingine ya kitamaduni.
Aidha Bwana Gao Wei ameeleza kuwa
mbali na maadhimisho hayo kufanyika Mnazi mmoja, pia yanatarajiwa
kuadhimishwa katika miji mingine ya Arusha, Dodoma na Mwanza katika siku
tofauti tofauti.
China ilianza kuadhimisha sherehe hizo tangu karne ya 12 ambapo kwa mwaka huu, kilele cha sherehe hizo ni February 8, 2016.
0 comments:
Post a Comment