Friday, January 15, 2016

 


 Mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, hayati Edward Sokoine, Namelock Sokoine amepita bila kupingwa nafasi ya mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Wilaya ya Monduli.
Nafasi hiyo iliachwa wazi na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyehamia Chadema.
Lowassa alijiengua CCM na kujiunga na Chadema na kugombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Elisante Kimaro alisema jana kuwa Namelock ambaye pia aligombea ubunge, katika jimbo hilo na kushindwa na mgombea wa Chadema, Julius Kalanga, amepita bila kupingwa kutokana na mpinzani wake, Lanyoni ole Supuku kutorejesha fomu.
Alisema katika nafasi ya mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, ambayo ilibaki wazi baada ya Reuben Ole Koney kuhamia Chadema, Loata Sanare amepita bila kupingwa.

0 comments:

Post a Comment