DEOGRATIUS MONGELA
MSANII wa Muziki wa RnB, Mtanzania mwenye maskani yake nchini Sweden,
Khairat Carlo Omar, ’Dati’ amemshirikisha kwenye songi lake Mkali wa
Bongo Fleva Sunday Mjeda ‘Linex’ na kumtumia tiketi ya ndege kwa ajili
ya kufanya video nchini humo.
Dati anayetamba na wimbo wake wa Can Do uliotengenezwa na Prodyuza
Fundi Samweli na video ikiwa imeshutiwa na wakali kama Hanscana na
Khalfan, ameweka mipango ya kufanya wimbo mpya na Linex ambapo alisema
kuwa wimbo huo ni ladha mpya kabisa kusikika Bongo.
“Mipango yote inaenda sawa na wimbo wangu na Linex utakuwa ni wa
Kiswahili, lengo la kufanya video huku Sweden ni kuutanua muziki wangu
na kukitangaza Kiswahili, hii ni kwa wale mashabiki wa Linex,” alisema
Dati.

0 comments:
Post a Comment