Mchekeshaji
wa Orijino Komedi na mjasiriamali, Masanja Mkandamizaji amesema kila
anachomiliki amekinunua kwa pesa yake halali huku akishangaa kwanini
watu wameshtuka baada ya kuona anamiliki BMW yenye plate namba ya jina
lake.
Akizungumza
katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii, Masanja alisema
anamiliki magari mengi huku akidai BMW X6 ameinunua kama mtu mwingine
anavyonunua baiskeli. "Mimi nina magari mengi sana na yote nayachukulia
kama chombo cha usafiri cha kunitoa point moja kwenda nyingine,”
alisema. “Sasa nashangaa watu wanaongea sana kuhusu mimi kwani gari kitu
gani! Hiyo BMW X6 nimenunua kama watu wengine wanavyonunua baiskeli,"
alijinadi.
Aliongeza, "Na hata hao TRA kama wananisikia waje hapa Clouds nimekuja nayo ipo hapo chini ili waangalie kama sijailipia." Masanja alisema anafanya biashara za aina mbalimbali hivyo kununua gari la thamani siku kitu cha ajabu kwakuwa anaweza kununua kupitia biashara yake moja tu.

0 comments:
Post a Comment