CHANDE ABDALLAH
MKALI wa nyimbo za harakati na aliyekuwa mgombea wa Ubunge kupita
tiketi ya Chama cha ACT, Kalama Masoud, ‘Kala Pina’ amefungukia sababu
za kumsifia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli
kupitia wimbo wake wa Magufuli Balaa.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Kala Pina alisema kuwa
japo kuwa yeye anatokea chama cha upinzani lakini hiyo haimaanishi kuwa
lazima apinge kila kitu na kudai kuwa amependa kasi ya utendaji wa rais
na yeye kama msanii ameona ni vyema kutoa wimbo huo ili kuelezea hisia
zake.
“Mimi ni mwanaharakati na harakati siyo upinzani ni kujenga nchi,
rais amenifurahisha nami kama msanii nimeamua kumtungia wimbo ili
kuelezea hisia zangu kwake siyo eti kwa kuwa mimi ni mpinzani nipinge
tu,” alisema Kala Pina.
0 comments:
Post a Comment