Posted by Williammalecela.com on Wednesday, January 06, 2016
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema
Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi
vilivyopendekezwa na waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo kasi Dar
es salaam (UDART).
Akizungumza leo na waandishi wa habari,
mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea mkoani Ruvuma kwa ziara ya
siku 3, Waziri Mkuu amesema Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli
ya mabasi yaendayo kasi. Ambapo nauli ya kutoka Mbezi hadi Kimara
shilingi 700, Mbezi hadi Kariakoo shilingi 1200, na nauli ya kutoka
Mbezi hadi Mwenge shilingi 1400 na wanafunzi watatozwa nusu ya viwango
hivyo vya nauli.
Waziri Mkuu amesema gharama hizi ni
kubwa mno kwa wananchi na watumishi, mradi ulilenga kumrahisishia
mtumishi wa Serikali anayeishi nje ya jiji,
“Serikali iliwekeza katika mradi huu ili kusaidia watumishi na wananchi ambao hawana vipato vikubwa” alisema Waziri Mkuu.
Aidha, ameagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George
Simbachawene na Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi, na Mawasiliano pamoja na
wadau wakutane kupanga upya viwango hivyo na kama watashindwa basi
Serikali itaendesha mradi huo.
Tarehe 25, Novemba 2015, Waziri Mkuu
alimuagiza aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya TAMISEMI na waendeshaji wa
mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART) kupitia misuada yote
na kurekebisha miundombinu ili mradi huo wa mabasi uanze kufanya kazi
ifikapo tarehe 10, Januari 2016, imebainika kwamba UDART hawakuandaa
mpango wa biashara wala kuanisha gharama za uendeshaji.
0 comments:
Post a Comment