Posted by Williammalecela.com on Friday, January 15, 2016
 |
| Le Mutuz Nation chini leo meeting Super Bilioneaz Davis Mosha and Super Bilionea Dr. Ndege Seba on matayarisho ya ufunguzi wa Radio na TV mpya African Swahili Media ambapo Radio Station itakuwa Morogoro na TV Station itakuwa Dar. |
 |
| @LE MUTUZ NATION LIVE STRAIGHT TALK!!:- Baada ya kuishi Belgium/Europe na New York City/USA kwa miaka 30 siku moja ghafla Miaka 5 iliyopita niliamua kurudi Bongo I mean home au nyumbani, ulikuwa ni moja ya uaamuzi mgumu kama ulivyokuwa uamuzi wa kwenda. Ulikuwa ni uamuzi mgumu sana kwa sababu baada ya Miaka 30 Majuu nilikuwa ninarudi nyumbani kufanya nini? Nitaanzia wapi? Nitaishia wapi? All I had at hand was USD $ 1,000 nilijiuliza mara nyingi sana within my self kwamba Miaka 30 Majuu what do I have to show I mean to justify all those years? Well, nilikuwa nimejisomesha Degree 3 na nimejenga nyumba na nina shamba la eka 4 Kinyerezi, nikajiuliza is that all? But nikajipa moyo kwamba kwenda kwangu nimejiongea kitu kimoja kikubwa na muhimu kuliko vyote nacho ni nimejongezea AKILI KUBWAZZ. Yes nimeongezeka sana Uwezo wa kufikiri kuliko ule niliokuwa nao kabla sijaenda Majuu, so nikaamua kwamba hicho peke yake ndio cha maana nilichonacho katika kuamua kurudi kwangu Bongo I mean home, so nikaamua kurudi. Nikamfahamisha my best and close Friend Peter Luangisa kwamba nimeamua kurudi Nyumbani na sitaki ushauri wowote unless ni kunishauri kuhusu kurudi tu, nikawafahamisha Wazungu Kazini kwangu Kampuni ya Stery Circle ni kampuni niliyokuwa nimeifanyia kazi kwa takribani miaka 25, ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona Mmiliki wa Kampuni yangu akitoa machozi. Mama wa kizungu alijaribu kila njia kunishawishi nibadili uamuzi wangu lakini nilimkatalia kata kata. Ninakumbuka mfanykazi mwenzangu Thomson kutoka Jamaica alivyopigwa na mshangao kumuona Mama Tajiri wa Kizungu akilia machozi, aliniambia "African Man, today is my first time to see A White folk crying for a Blackman, you must have been bringing them good money" Mama wa kizungu akanipa Wiki Mbili kupumzika kwanza na malipo ili nifikirie tena kama kweli ninataka kuondoka, nikamkatalia kata kata, aakamua kunipa pesa za malipo ya Wiki 3 za kazi bure na akanipa ahadi nzito sana kwamba kama ningerudi kazini in one year nitaikuta nafasi yangu ya kazi ipo pale pale pamoja na Senority yangu, na iwapo ningerudi after one year ataniajiri upya lakini all and all nafasi Mzungu alinihakikishia kwamba nafasi yangu ya kazi ipo pale pale as anaishi na anamiliki ile kampuni. Mama wa Kizungu tena akanihakikishia kwamba nikitaka kurudi America nimfahamishe tu atanilipia nauli na kunitafutia viza. Ninakumbuka ilikuwa almost kama siku ya kilio Wafanyakazi wenzangu wote walipotangaziwa kwamba kesho yake Ijumaa ingekuwa siku yangu ya mwisho pale kazini na kwamba kila mfanyakazi alitakiwa kuja mapema Saa Moja Asubuhi kuja kuagana na mimi "AFRICAN BILLY BOY" kama walivyokuwa wakiniita. Kesho kwa mshangao mkubwa Wafanyakazi wenzangu wengi walijitokeza na wake zao na watoto wao kuja kuniaga "African Billy Boy" au "A Solid Human Being" alivyokuwa akiniita Mama Mzungu mwenye kampuni. ilikuwa ni siku ya huzuni sana I had to cry kwa kawaida mimi huwa ni binadam mgumu sana kutokwa na machozi but I had to, sikujua kwamba I had that much impact na my co-workers, wengi wao walisema nilikuwa ni binadam wa kwanza wa aina yangu waliyewahi kukutana naye maishani mwao nilipiga picha nyingi sana nao na mabosi wangu wote na wakanipa zawadi nyingi sana. Kesho yake Mchana Saa Nane ilikuwa siku ya Jumamosi My friend Peter Luangisa akanipitia tayari kwa safari ya kuelekea John F. Kennedy tayari kupanda Swiss Air kurudi home Bongo......Itaendelea Next Week | | |
Duu kweli kaka una moyo unanipa moyo sana hata mimi niko Europe takriban 19 years ila nataka kurudi nyumbani napenda sana nchi yangu nitarudi kaka sioni ugumu home hata ugali unakula huku unajenga maisha cha msingi pa kuingia ukifika kupo uschekwe na wenye midomo mirefu tu. Nasubiria kwa hamu sehemu ya pili Lemutuzz Nafwaaaa wallah.
ReplyDeleteThis is so heartbreaking and encouraging. Im in the same position cant wait to read the next part.
ReplyDelete