Jana
mmoja ya Viongozi wa shrikisho la Vyuo vikuu CCM Ndugu Ally S. Hapi
alitoa TAMKO Zito la kumtaka Mwanasiasa na Kada wa CCM MNEC Bernad Membe
aache kumkosoa Rais wa Jamhuri John Pombe Magufuli kuhusu kufuta safari za nje
na kuhusu ukubwa wa Baraza la Mawaziri.
Hata hivyo baadae
iliibuka taarifa moja kwenye Mitandao ya Kijamii kilichoonekana kuwa ni
TAMKO la mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bi Zainab Abdallah.
YAH: KUKANUSHA TAARIFA ILIYOTOLEWA
KWA JINA LANGU
Nimepokea Na kuona taarifa
inayozunguka Katika mitandao ya Kijamii ikionekana kuwa imetolewa Na Mimi Kama
mwenyekiti wa Shirikisho. Taarifa Hiyo yenye jina langu inaeleza kuwa nimepinga
Na kukanusha taarifa ya Kiongozi Mwenzangu Wa Shirikisho ambaye awali alikuwa
ametoa Taarifa yenye Maudhui ya Kumjibu MNEC Benard C. Membe.
Napenda kuwataarifa Watanzania wote
kuwa Mimi mwenyekiti wa Shirikisho sijatoa Taarifa yeyote Leo hii Na wala
sijashiriki kikao chochote Cha Shirikisho ambacho ndio kinanipa Jambo lolote la
kulitolea Taarifa.
Napenda ieleweke kwa Watanzania
wenzangu wote kuwa Uongozi ni Vikao. Mimi nikiwa Kama Mwenyekiti wa Shirikisho
nitatoa taarifa yeyote baada ya Kukaa Na Wajumbe wenzangu kwa mujibu wa Kanuni
zetu. Hivyo wananchi Mtambue kuwa taarifa iliyotolewa kwa jina langu siijui Na
siyo yangu bali ni ya kutungwa tuu Na watu ambao sielewi malengo Yao ni nini.
Mwisho napenda kuwaomba Watanzania
wote tuendelee kumuunga Mkono Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ili
aendelee kuwaletea mabadiriko Watanzania Kama alivyoahidi.
Nawashukuru sana Na nawatakia
Ujenzi Mwemba wa Taifa.
M/kiti wa Shirikisho Taifa,
Zainab Abdallah
24.Januari 2016

0 comments:
Post a Comment