Saturday, February 6, 2016





Msanii wa Kundi la Yamoto Band, Aslay amesema kifo cha mama yake mzazi kimewapelekea waimbe wimbo ‘Mama’ kuwaenzi akina mama wote.
Aslay2

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Aslay alisema yeye pamoja na msanii mwenzake katika kundi hilo ‘Enock’ wamewapoteza mama zao siku za karibuni ndipo wakaamua kuwakumbusha watanzania umuhimu wa mama.

“Unajua mimi na mwenzangu Enock tumewapoteza mama zetu siku za karibuni hivyo tuliamua kuwaimbia kina mama kwa hisia kali ili kuwaenzi wakina mama wengine na kuwakumbusha watanzania umuhimu wa mama na kuwatahamini, maana sisi wenzenu tunalia kwa kuwapoteza kina mama. Lakini kiukweli wimbo huu (Mama) ninapo usikiliza napata raha na kufarijika kwa kile tulichokifanya,” alisema Aslay.
Aidha, Aslay amesema tayari wameshashoot video ya wimbo huo mkoani Tanga na sasa ipo katika hatua za mwisho ili itoke.


0 comments:

Post a Comment