Blac Chyna
IMEBAINIKA kuwa mwanamitindo na mcheza utupu, Blac Chyna yupo katika
mipango ya kujiachia kimapenzi na mdogo wa mwanamitindo, Kim Kardashian,
Rob katika sikukuu ya Valentine’s Day wiki ijayo.
Rob na Blac Chyna
Chanzo makini kilianika ubuyu kuwa Blac anayo furaha kubwa kuwa
kimapenzi na Rob na kwamba anachotaka siku ya wapenda nao (Valentine’s
Day) kuona wakitoka sambamba na ukoo wa Kardashian.
“Anayo furaha kuona wakitoka kama kundi la familia na kwenda
kushiriki katika sehemu maalum. Anataka kuwepo na Rob, Kim na Kanye,
Kylie na Tyga, Kris na Corey, Khloe na James,” kilisema chanzo.
Blac Chyna awali alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na rapa Tyga
na kufanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja, King Cairo. Kwa sasa Tyga anatoka
na mdogo wa Kim Kardashian, Kylie Jenner.

0 comments:
Post a Comment