Msanii wa Hip Hop wa Kundi la Weusi, Joh Makini ameeleza sababu mbalimbali zinazowasukuma wasanii wanaotoka mikoani kufanya vizuri kimuziki pindi wanapofika Dar es Salaam.

Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na video ya wimbo ‘Don’t Bother’ akiwa amemshirikisha AKA, amekiambia kipindi cha Mkasi TV
kuwa wasanii wengi wa mikoani hufanikiwa kutokana na kujiona wako mbali na nyumbani.
“Unapokuwa umetoka kwenu ukaja sehemu kufanya kazi, lazima ujue hapa sio kwenu umekuja mjini. Kwahiyo lazima uhakikishe kwanza speed yako sio ya kawaida katika kazi,” alisema Joh.
“Mimi wakati nimekuja Dar, nilikuwa naishi geto, na tulikuwa tunaishi kwa kubangaiza mizinga mingi na nini. Unapokuwa unaenda studio na kurudi geto, unajua sio kwenu pale unaamshwa muda wowote. Huwezi kufanya kazi katika speed ya kawaida kama ni mtu unapenda na unakijua unachokifanya. Kwahiyo mimi nafikiri labda wasanii wanaotoka mikoani wanakuja Dar es salaam wengi wanafanya vizuri kwa sababu kuwa mbali na nyumbani inakusukuma kufanya kazi kwa bidii kwa sababu upo hapo kwa wakati na unatakiwa kuitumia kila dakika,”
Joh Makini ambaye anatoka Arusha pamoja na wasanii wenzake wa Kundi la Weusi, ni miongini mwa wasanii wa Hip Hop wenye makanikio kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment