Thursday, February 25, 2016


Kondakta wa basi la Masimba Exress akiwa eneo la tukio

Basi la Mashimba Expess likiwa limeharibika
Mashimba Express


Gari ndogo

Watu wane wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la Mashimba Express lililokuwa linasafiri kutoka Kahama kwenda jijini Mwanza kugongana na gari dogo  katika eneo la njia panda kuelekea wilayani Kishapu.

Ajali hiyo imetokea leo jioni ambapo mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa gari ndogo ilikuwa katika mwendo kasi na watu wawili kutoka katika gari hilo akiwemo dereva amefariki dunia.

Malunde1 blog imefika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na kushuhudia baadhi ya majeruhi wakipatiwa matibabu.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt Albert George Masigati amesema kati ya saa 12 na saa moja usiku huu wamepokea miili ya marehemu wanne katika hospitali hiyo ,wote ni wanaume na majeruhi wanane,kati yao wanawake wanne na wanaume wanne.

Hata hivyo Dkt Masigati amesema huenda idadi ya majeruhi ikaongezeka kutokana na taarifa kuwa baada ya ajali hiyo kutokea baadhi ya majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya Kolandoto na Kishapu.

Dkt Masigati amesema hakuna majeruhi aliye katika hali mbaya na kwamba bado wanaendelea kuwafanyia uchunguzi kutokana na kwamba wamepata michubuko mbalimbali katika miili yao.

Mmoja wa abiria katika basi hilo aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhan aliyelazwa katika hospitali ya rufaaa ya mkoa wa Shinyanga amesema basi lao lilikuwa katika mwendo wa kawaida lakini gari dogo ndiyo lilikuwa katika mwendo kasi.

Tutawaletea taarifa kamili hivi punde,bado tunafanya jitihada za kumpata kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya taarifa zaidi kwani namba zake za simu hazipatikani.
 

Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

0 comments:

Post a Comment