Watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi mkali. |
Watuhumiwa wanne kati ya tisa wanaotuhumiwa
kuhusika na tukio la kutungua helikopta iliyokuwa ikifanya doria kwenye pori la
akiba la Maswa wilayani Meatu Mkoani Simiyu na kumuua rubani wake, wamehukumiwa
kifungo kwenda jela miaka 70.
Baada
ya maelezo ya wakili huyo mahakamani hapo, watuhumiwa wote wanne kati ya saba
walikiri kutenda makosa hayo, ambapo wote waliiomba mahakama kuwapunguzia
adhabu kwa kile walichoeleza kuwa ni mara yao ya kwanza kutenda makosa kama
hayo.
Hata
hivyo wakili Mlekano aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa wote
ili kuwa fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutenda makosa kama hayo.
Hata
hivyo Hakimu Mrio alieleza kuwa katika kosa la tatu ambalo watuhumiwa wawili
kati ya hao saba walikiri kutenda, mahakama imewahukumu kifungo cha miaka
mitano (5) jela kila mmoja au kulipa faini ya shilingi Milioni 10.
Kwa
pamoja watuhumiwa wote wanne watatakiwa kutumikia kifungo jela miaka 70, huku
baadhi yao wakitumikia kila mmoja kifungo cha miaka 20 na wengine kifungo cha
miaka 15 kila mmoja.
0 comments:
Post a Comment