Na Happiness Katabazi
KWA wiki Tatu sasa kuna kitu kinanisukuma niandike Kuuliza Swali hili ; "
CCM inakumbuka familia ya aliyekuwa kiongozi wa bendi wa TOT,marehemu
John Komba?
Kabla ya kampeni za uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 niliiandika Wimbo wa CCM
Mbele Kwa Mbele Uliotungwa na Komba na nilitabiri Kuwa Wimbo huo
utakuja Kuwa ni Wimbo maarufu wakati wa kampeni zikianza na utaibeba
sana CCM na ndivyo ilivyokuwa Kuwa Kwani Wimbo ulikuja Kuwa maarufu sana
ndani na nje ya nchi kutokana na Maudhui yake.
Hivyo kuisababishia CCM kuzidi kupata mashabiki Wengi na hata kuna
baadhi ya watu waliokuwa wameichukia CCM, kupitia Wimbo huo wa CCM
Mbele kwa Mbele Walijikuta wakianza kuipenda CCM na kuweka Wimbo huo
Kwenye miito ya simu zao za mikononi,pikipiki,Kwenye Magari,kompyuta na
baadhi ya maneno yaliyomo Kwenye Wimbo huo ya natumiwa mitaani na baadhi
ya watu kufikisha ujumbe Fulani.
Lakini kwa bahati Mbaya Mtunzi wa Wimbo huo Komba alifariki mapema Kabla
ya Wimbo wake aujaanza kupigwa Kwenye kampeni na hivyo haukuweza Kuwa
Shuhuda wa jinsi Wimbo alioutunga ulivyojizolea Umaarufu.
Komba Enzi za Uhai wake alitunga nyimbo nyingi ambazo ziliiletea sifa
CCM na ushindi pia. Wimbo wa CCM Mbele kwa Mbele tulishuhudia aliyekuwa
mgombea urais wa CCM ambaye kwasasa ndiye rais wa Tanzania, Dk.John
Magufuli alipokuwa jukwaani akinadi sera zake alikuwa akiutumia wimbo
huo kupiga push up , kucheza kwa madoido Hali iliyosababisha na yeye
kujiongezea wa shabiki wake ambao walimpa kura .
Je ,Rais Magufuli na Makamu wako wa Rais, Samia Suluhu maana ndiyo mmpo
madaraka kwasasa na Wimbo huo ilitumika hasa kuwanadi wewe
Magufuli,Samia na wabunge hivi mlishawahi kukaa chini kila mtu kwa
nafasi yake minafikiria kwenda kumjulia Hali familia ya marehemu Komba
nyumbani kwake au hata basi mmuite Mkewe ofisini wake mmjulie Hali ?
Au ndiyo mtasema mpo Bize sana na kufukuza watu kazi,kuwasimamisha watu
kazi,kuamrisha Polisi wakamate watu wahalifu, kuvunjia nyumba wakazi
wazi wa mabondeni na kufanya ziara za kushtukiza?
Ni Mwendawazimu peke ya anayeweza Kusema wimbo wa CCM mbele kwa Mbele
haukuchangia ushindi CCM. Kama CCM mna ikumbuka familia ya Komba Mungu
awabariki ,ila kama hamuikumbuki familia yake itakuwa siyo jambo Jema
na mtalaaniwa.
Nimesema hayo kwasababu wanasiasa Wengi wanatabia Moja Mbaya sana
wanamtaka mtu na kumthamini mtu kinafki pale wanapokuwa wanaitaji ajenda
Yao ikamilike kupitia mtu Fulani,akishafanikiwa hawana wanahabari nae.
Komba mchango wako wa utunzi, uimbaji hautasaulika ,umeacha harama ya
kuigwa hasa sauti yako ambayo hadi sasa bado haijapatikana mtu wakuweza
kuiga sauti yako.
Mungu ibariki Tanzania
0716 774494
Chanzo:Facebook.Happy Katabazi
Blogg: katabazihappy.blogspot.com
30/12/2015

0 comments:
Post a Comment