"Leo
nimetembelewa na Balozi wa Ufaransa na ujumbe wake. Tumekuwa na
Mazungumzo mazuri sana.
Nimemweleza juu ya shauku yetu ya ujenzi wa Machinjio ya kisasa na kuwa wilaya yetu imeshatenga eneo la hekari 55 na michoro ya ujenzi imeshakamilika na ujenzi ukifanyika Ng'ombe 900 na mbuzi 860 watachinjwa kwa siku moja kutokana na utafiti unavyo onyesha mahitaji ya nyama kwa siku moja hapa mjini. Pili nimemweleza juu ya ujenzi wa Centre ya Vijana watakaojifunza mambo ya kilimo na ufugaji na eneo tumeshatenga zaidi ya heka 40.Faida ya Miradi hii miwili ni kubwa sana ikiwezo kuwa na nyama yenye ubora, usafi, mapato yatokanayo na Machinjio, kiwanda cha Ngozi, Ajira na zaidi ni maendeleo kwa Wilaya yetu. Balozi na ujumbe wake wameonyesha nia ya Kusaidia na wamefurahi kuona miradi inayogusa maisha ya wananchi wote."

0 comments:
Post a Comment