Saturday, February 13, 2016

Maua sama
Msanii wa bongo fleva Maua Sama amefunguka na kusema kuwa ameamua kujikita zaidi kwenye muziki hasa baada ya kumaliza chuo.Maua amesema kwa sasa hafanyi shughuli yoyote zaidi ya muziki na kikubwa na anataka kutumia elimu aliyoipata ya mambo ya ‘Makerting and Enterprenurship’ ili aweze kujikuza kisanaa.

Nilikuwa mwanafunzi,sasa nimemaliza chuo nimeamua kujikita kwenye muziki kwa asilimia mia moja…kwa sasa hakuna shughuli nyingine nayofanya nataka nitengeneze ‘base’,nifike malengo yangu kimuziki halafu nione nitatumiaje jina langu na elimu niliyo nayo kutengeneza hela zaidi maana uzuri wake mimi nimesoma makerting and enterprenurship kwa hiyo kwa kazi nayofanya ya muziki naweza kutumia elimu yangu kujifikisha mbali zaidi” alifunga staa huyo wa ‘So crazy’.
Pia kwa upande mwingine Maua amesema mikakati yake kwa sasa ni kuufikisha muziki wake kwenye level za kimataifa zaidi.
Source:Global Online Tv

0 comments:

Post a Comment