Sina uhakika kama Diamond na Rommy waligombana lakini kwa habari za
chini chini inasemekana kuwa Rommy na Diamond walitofautiana ingawa wao
hawakuthibitisha hilo!
Taarifa za chini chini zinasema kuwa Rommy na Diamond walitofautiana
baada ya Rommy kuambiwa ajitegemee! Ndipo Rommy alipo kaa mbali na WCB
na kuamua kuanza kurusha Matangazo katika Ukurasa wake wa Insta!
matangazo yalio kuwa yana muhusu diamond alikuwa anatoa kwa kuibia ibia
sana
Ikumbukwe kuwa show za Diamond zote Rommy alikuwa ndio Dj lakini baada
ya kutofautiana kwao hakuonekana tena kwenye show hadi Usiku wa Mkesha
wa Valentines day ambapo Diamond Alifanya Show kubwa Kisumu Kenya
Wakiwa na Crew ya WCB kenya Rommy ameonekana kwenye picha ya pamoja
jambo ambalo watu wamesema ni kutokana na kumaliza tofauti zao na hivyo
ataendelea kuwa Dj wa Diamond katika show zake zote
Juzi Rommy alipost videos mbili zikionesha akiwa kwenye Ndege kuelekea
kenya ingawa yeye hakusema kama anaende kenya ndipo Esmaplatnumz alipo
comment na kusema nakuona Rommy Nairobi Moja!
Diamond nae alipost video akionesha anatoka SA kwenda Kenya kwenye show!
Ule usemi wa kuwa Ndugu wakigombana Shika Jembe ukalime ni dhahiri kuwa umetimia!
Sasa Diamond + Rommy wapo pamoja tena na Kazi zinaendelea! kama ni kweli waligombana Hongera kwa alie wapatanisha!


0 comments:
Post a Comment