Thursday, February 4, 2016


Msanii Shilole ametoa ushauri kwa wasanii wa kike pamoja na mbinu mbalimbali ambazo zitawafanya kuwa wasanii wakubwa wa muziki.
Muimbaji huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wa kike wenye mafanikio kwenye muziki, amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa, ili msanii afanikiwe anatakiwa kujitume zaidi.
“Wasanii wengi wa kike wanashindwa kufika pale wanapotaka kwa sababu hawako serious,” alisema.
“Mimi kazi yangu naifanya ndio kila kitu, bila kuimba vizuri, bila kudance vizuri, bila kufanya video kali, watoto wangu watakufa njaa. Unajua sometime wasanii wa kike tunajibweteka tukishatoa ngoma moja tunaona hii ndio itanivusha 2016, hapana unatakiwa uendelee kukomaa yaani kila siku wewe uwe ni mtu wa kuangaika kurecord kazi mpya, kwa sababu lazima uwe na ngoma nyingi kwenye library ili ukitaka kutoa ngoma unachagua moja kali,”

Aliongeza “Kitu kingine tusibweteke na umaarufu tunaopata, tufanye kazi, vilevile tuwe tunatunza pesa ambazo tunapata. Pia tusitegemee kabisa wanaume, kwa sababu ukishakuwa maarufu wanaume wengi watakufuata, sasa unatakiwa ujitambue wewe ni nani,”

0 comments:

Post a Comment