Mwimbaji wa bongo fleva anayetamba na wimbo wa kwa Hela Linex amefunguka na kusema kuwa tofauti ya kuwa na mpenzi wa kibongo na wa kizungu ni kwamba wazungu wako ‘real’.
Msanii huyo ambaye amewahi kutoka kimapenzi na demu wa kizungu na sasa yuko na demu wa kibongo amefunguka na kusema kuwa mademu wengi wa kibongo ni pasua kichwa ndio maana watu hawadumu.
“Tofauti ya mapenzi ya kibongo bongo na wazungu iko kwenye uwazi au ukweli..wenzetu wako real.Wabongo longo longo nyingi kudanganyana sana ndo maana watu wanakaa wiki mbili wanaachana” alifunguka msanii huyo na kuongeza kuwa hakuna kitu kikubwa kwenye maisha kama ‘trust’.
Source: cloudsfm
0 comments:
Post a Comment