MSIBA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI , KIKANDA NA KIMATAIFA .
wanasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wao Bw. Manfred Ngatunga kilichotokea jana tarehe 14 Feb 2016 huko Mkata akiwa njiani kuelekea Muheza , kwa mshituko wa Moyo.
Tarehe 12 Feb 2016 siku ya Ijumaa Bw. Ngatunga aliangwa rasim na watumishi wenzake wa Idara ya Uhasibu alipokuwa akijiandaa kuanza likizo ya kustaafu utumishi wa umma leo Jumatatu tarehe 15 Feb 2016 baada ya kulitumikia taifa kwa kipindi cha miaka 38. Msiba upo Muheza Mkoani Tanga na anategemea kuzikwa hukohuko Muheza siku ya Jumatano tarehe 17 Feb 2016. Bwana Ametoa Bwana ametwaa jina lake liimidiwe.


0 comments:
Post a Comment