Promota maarufu kutokea mkoani Ruvuma amedai kwamba Msanii wa bongo fleva ambaye pia ni diwani wa kata moja huko Kigoma,Baba Levo amemdhurumu pesa zake kiasi cha shilingi laki tatu ambazo alimkopa kumlipia mwanae ada ila akawa mgumu kulimpa.
“Baba Levo alikuja akaniambia nina shida ya pesa,mtoto hana hela ya shule kwa kuwa huko kwao kigoma hela hazijaingia,mwisho wa siku namdai ananitumia meseji za ajabu ajabu mara oh kachukue hela kwa Shilole“alifunguka Promota huyo na kuongea hata Shilole alimlalamikia kuwa ameweka bondi gari lake (gari la Shilole)
Alipoulizwa Baba Levo alifunguka haya “Nimemdhurumu huyo kwa kuwa nimemzidi kila kitu hadi nguvu,aende mahakamani akafungue kesi.Mtu akidhurumiwa hela anaenda kwenye vyombo vya habari au mahakamani” alifunguka Baba Levo ambaye baadaye aligeuka na kusema kwamba Promota hajampa chochote na yeye ana mijihela ya kutosha ila amepanga kumchafua kwa kuna matatizo baina yao na kuongeza kuwa yeye hachafuki ng’o.

0 comments:
Post a Comment