Wednesday, March 16, 2016


Baada ya Simba kuendelea na malalamiko ya muda mrefu kuwa klabu ya Dar Es Salaam Young African inapendelewa na shirikisho la soka Tanzania TFF kwa mambo kadhaa, ikiwemo wachezaji na viongozi wake kutopewa adhabu. Mchana wa March 16 mkuu wa idara ya habari wa Yanga Jerry Muro ameweka wazi suala hilo.

Jerry amelazimika kuweka wazi kwa wanaosema kuwa yeye amemkosea msemaji waSimba na anatakiwa kuadhibiwa, wanakosea kwani kama angekuwa amekosea angeshitakiwa katika vituo vya polisi, kwa sasa anaomba wasiiandame Yanga kwani ina mechi za kimataifa.
“Sisi tunajiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya APR tutakaocheza jumamosi, lakini jamani sisi kama Yanga tunaomba watuache wasituandame na maneno maneno, tupo katika mashindano ya kimataifa, kuhusu kuhairishwa mechi hiyo inatokana na sisi kucheza mechi za kimataifa” >>>Jerry Muro

0 comments:

Post a Comment