Saturday, March 19, 2016



Muimbaji wa ‘Looking For You’, Jux amedai kuwa mzigo wa kwanza wa nguo zake za African Boy uliisha ndani ya saa 24.

Akiongea kwenye kipindi cha The Sporah Show, Jux amedai mwanzoni alitengeneza t-shirt 200 tu kusoma mchezo kwanza lakini alishangaa kuona zikiisha katika muda mfupi sana.


Anasema t-shirt zake zina bei kidogo kuanzia shilingi 35,000 lakini baada ya kununuliwa na kumalizika katika muda huo alipata moyo wa kufanya mambo mengine makubwa zaidi.

Akiongelea kuhusu jina la African Boy, Jux alisema lilikuja baada ya kugundua kuwa watu wengi katika chuo anachosoma China walikuwa hawaamini kama anatokea Afrika.

Alisema aliamua kuanzisha brand hiyo kwasababu anaipenda Afrika na alipenda watu wajue hivyo.

0 comments:

Post a Comment