Hakuna tofauti kabisa kati ya kile Shaa amezungumzia kuhusu yeye na Vanessa Mdee na jinsi vyombo vya habari vinavyojaribu kuwashindanisha kwa lazima. Rihanna na Beyonce wamekuwa wakikutana na hali hiyo pia japo wapo sababu ni tofauti kidogo kwakuwa inahusisha madai ya Riri kuwahi kuwa na uhusiano na mume wa Queen B, Jay Z.
Kwenye mahojiano na jarida la Vogue, wamezungumzia single ya kushtukiza ya Beyonce “Formation” iliyotoka wiki ambayo Rihanna aliachia album yake Anti na kama ndio sababu mashabiki wameendelea kuwashindanisha.
Rihanna anadai hilo halimsumbui.
“Iko hivi. Wanafurahia tu kusherehekea kwenye kitu ambacho ni hasi,” anasema Rihanna. “Kitu ambacho ni cha ushindani. Kitu ambacho unajua, uadui. Lakini hicho sio kitu ambacho naamka kwaajili yake. Kwasababu naweza kufanya kama mimi tu. Na hakuna mtu mwingine ataweza kufanya hivyo.”
Kwa upande mwingine Rihanna ambaye yupo kwenye ziara ya dunia ya majiji 63, amesema ratiba yake ngumu inamfanya ashindwe kuwa kwenye uhusiano. “Ratiba yangu ni ngumu sana sasa. Ni wazi itakuwa changamoto pale nikiamua kuanzisha uhusiano, ila nina matumaini.”
Pia anasema ajivunia na album yake mpya pamoja na kwamba haijawa maarufu kama zilizopita.

0 comments:
Post a Comment