Hapa yapo Aliyosema Meneja wa Diamond kuhusu kufanya kolabo na Kanye West.
Ni
Siku chache baada ya msanii Diamond platnumz kupost picha kwenye
instagram akiwa na kanye West ambaye ni rapper mashuhuri ulimwenguni
watu wengi wamekuwa wakihisi pengine kuna kolabo inaweza kutokea hasa
baada ya kusemekana wasanii hao walibadilishana namba.
Akihojiwa
na moja ya kituo cha redio moja mmnoja wa mameneja wa Diamond,Sallam
amesema kuwa huwezi kufanya kolabo na msanii kama kanye West kisa
umekutana naye tu kwani kuna protokali nyingi zinabidi zifuatwe mpaka
kukamilisha hilo na kuongeza kuwa kwa CV ya Diamond nafasi inaweza
kupatikana.
“unajua
wenzetu hawafanyi kolabo kwa sababu umekutana naye,lazima utengeneze
kuwa wewe ni nani,ukifanya naye kolabo itamsaidia nini yeye,nashukuru
kwa upande wetu tuna Cv nyingi kwa hiyo nadhani itatusaidia kwa upande
mwingine” alifunguka Sallam.

0 comments:
Post a Comment