Saturday, March 26, 2016

khadija kopa
Malkia wa muziki wa taarab nchini, Khadija Kopa amedai wasanii wengi wapya wa muziki wa taarab hawana heshima kwa wakubwa wao.
Akizungumza katika kipindi cha Uhondo cha EFM hivi karibuni, Khadija amesema hali hiyo imewafanya washindwe kufanya vizuri kwenye muziki wao.
“Unajua mimi watu wengi huwa wananiogopa, sijui ni kwa ajili ya hivi ninavyoimba mipasho ndio wanadhani labda mimi ni mkali. Lakini mimi siko hivyo kabisa, mimi ni mtu poa sana. Kwa hiyo hawapendi kunifuata, wananipigia simu au wanatuma meseji tu,” alisema Khadija.
Aliongeza, “Mara nyingi nikikutana na wasanii wa kike huwa nawashauri na kuwapa moyo juu ya maisha ya muziki. Lakini vijana wetu wengi wa sasa hivi hawana busara kusema ngoja nimfute mtu mzima atanielekeza njia za kupita, wengi wanajifanya wanajua ndio maana wanapotea mapema. Sisi tupo mpaka leo kwa sababu tuliongea vizuri na tuliowakuta kwenye game,”

CHANZO  na Bongo5.

0 comments:

Post a Comment