Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Madee Ali amesema Dogo Janja alimletea nyimbo zaidi ya 20 kabla ya kuupata wimbo ‘My Life’ ambao amedai huo ndio ulikuwa unaendana na soko.
Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Madee amesema alifanya yote hayo ili kumtaka Dojo Janja mpya.
“Unajua muziki ambao alikuwa anaufanya Dogo Janja mwanzo ulikuwa wa mkumbo fulani hivi, kwa hiyo watu wakaimba imba sana muziki huo” alisema Madee.
“Sasa alivyokaa kwa muda mrefu nilikuwa natafakari the way atavyorudi. Nikawa nawaza kusema arudi tena kwa mtindo wa zamani watu wasinge mwelewa. Dogo Janja ameniletea nyimbo zaidi ya 20, kila siku anarekodi lakini mimi namwambia bado, alivyoniletea My Life nikamwambia hapa safi, tukaedit kidogo ngoma ikatoka,” aliongeza Madee.
Pia Madee alisema anajipanga kuachia video ya wimbo huo hivi karibuni.

0 comments:
Post a Comment