Mabula
ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika mahojiano na kipindi cha
Hot Mix kinachorushwa na kituo cha EATV kila siku ya Jumatatu hadi
Ijumaa, saa moja jioni."Meya kweli ametoka upinzani ila kuwa Meya wa
jiji la Dar es salaam siyo kazi kubwa kwa sababu hata vyanzo vyake vya
kukusanya mapato sii vingi hapa atakusanya zaidi kwenye 'packing' ya
magari (ushuru wa maegesho)".Mabula ameongeza kuwa cheo cha umeyawa Dar
es salaam kimekaa kisiasa ndiyo maana hata alivyokuwepo Dkt. Didas
Masaburi kazi yake ilikuwa ni kushiriki kwenye shughuli za kitaifa na
kwenda kupokea wageni uwanja wa ndege wanaokuja kufanya ziara hapa
nchini.
"Kwa Dar es salaam, kila kitu kiko chini ya manispaa,
jiji halimiliki kitu, halimiliki shule, wala barabara na hata vyanzo
vyote vya mapato vinamilikiwa na manispaa tatu ambazo ni Temeke, Ilala
na Kinondoni
Meya wa jiji hana kauli yoyote kwa rasilimali karibu
zote za maendeleo"Mabula ambaye alikuwa Meya wa Jiji la Mwanza kabla ya
kuchaguliwa na wananchi kuwa mbunge wa jimbo hilo amesema katika
kipindi chake akiwa Meya,aliweza kutumia vizuri fedha za
maendeleokujenga barabara kutoka Mkuyuni kwenda Butimba kilomita 18
pamoja na kujenga tanki kubwa la maji eneo la Kishiri ambalo linahifadhi
maji zaidi ya lita laki mbili pamoja kuelekeza fedha za serikali miradi
mingine.
Aidha mbunge Mabula ambaye yupo katika Kamati ya Hesabu
za Serikali (PAC) ameeleza kusikitishwa kwake kwa baadhi ya kamati
kuanza kukumbwa na kashfa za rushwa na kupelekea baadhi ya wabunge
kujiuzulu na kusema kuwa hali hiyo haioneshi picha nzuri katika
kuwatumikia wananchi.

0 comments:
Post a Comment