Kufuatia
madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja amekuwa na katabia
ka’ kujiweka kimahaba kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakati Zarinah Hassan
‘Zari’ akiwa Sauzi, madai yametua mezani mwa gazeti hili kuwa, kimenuka
kati ya Zari na Kajala.
Chanzo chetu makini ambacho kimeomba jina
lake lisitajwe gazetini kimedai kuwa, hivi karibuni baada ya Zari kupata
ubuyu huo wa kuchovyewa penzi lake, alitafuta simu ya Kajala kisha
kumpigia na kumpa makavu kuwa, asimuingilie kwenye himaya yake.
0 comments:
Post a Comment