Mjane Manka Dominick akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu huku akiwa katika hali ya simanzi na mwanae baada ya kufanyiwa kitu mbaya na ndugu wa marehe
mu mume wake.
Mtoto akijiraza kitandani baada ya kulalamika njaa inamuuma.
Mwandishi wa
Mtandao huu aligushwa na kuamua kumpatia kiasi kidogo cha pesa dogo huyo za kununua Chips kwa muda wa siku mbili tatu.
lna um asana. Mjane Manka Dominick[28] mkazi wa kiwanja cha ndege Manispaa ya Morogoro aliyefiwa na mumewe Juma Kambaya hivi karibuni amefanyiwa kitu mbaya baada ya kunyang’anywa vitu vyote alivyochuma na marehemu mumewe.
Akiwa na Mtoto wa miaka minne aliyeza na marehemu,mjane huyo alisema ndugu wa karibu wa mumewe aliyefahamika kw ajina moja la Kassim alifika nyumbani kwa mjane huyo na kuchukua vitu vyote akidai mila na desturi zao zinaelekeza hivyo.
”Nilifunga ndoa na muwe wangu miaka 6 iliyopita na kujaliwa kupata mali na mtoto mmoja mwenzi uliopita Mpenzi wa Moyo wangu baba watoto wangu alitangulia mbele za haki baada ya kuugua kwamuda mfupi”alisema Manka na kuongeza.
“ Cha ajabu hata Arobaini bado mtu huyo kaja hapa nyumbani na kuchukua vitu vyote nilivyochuma na mume wangu na kuacha chumba cheupe akidai kwamba mila za kwao zinaelekeza hivyo,mimi na mwanangu tumelala chini wiki moja juzi jirani yangu ameniazima Kitanda na godoro ndio tunalolalia lakini kula yetu ni shida kama unavyomuona mwanangu amelegea kwa njaa haja pata chochote toka asubuhi”alisema Mjane huyo huku akitokwa na machozi.
Mtandao huu ulimtafuta ndugu huyo wa karibu anayedaiwa kuwa ni dereva wa boda boda anayefanya shughuliza zake katika kijiwe cha Tangi Bovu lakini alipomuona Mwandishi wa Mtandao huu aliwasha pikipiki yake na kuondoka huku akimwambia atarejea muda si mrefu lakini hata baada ya saa moja kupita hakurudi.


0 comments:
Post a Comment