
Fatuma Makame ‘Joanitha
Staa
wa Filamu Bongo, Fatuma Makame ‘Joanitha’ na Video Queen Gift Stanford
‘Gigy Money’ wanatarajia kuchuana kwenye filamu watakayocheza pamoja
hivi karibuni baada ya Gigy kuchukuliwa na Kampuni ya Hamadombe kwa
majaribio.
Akizungumza na Ijumaa, Joanitha ambaye ni bosi wa
kampuni hiyo alisema wamebaini Gigy anao uwezo mzuri wa kuigiza lakini
hajapewa nafasi hivyo wameona wakati anaendelea na U-Video Queen wake
pia acheze filamu.
Gift Stanford ‘Gigy Money’
“Unajua
kwa sasa tumeamua kuwachukua wasanii kama ‘brand’ ili kushindana na
makampuni mengine kwenye uigizaji hivyo tumemchukua Gigy Money na Tiko
Hassan ambao wataingia kambini muda si mrefu,” alisema Joanitha.

0 comments:
Post a Comment