Msanii wa muziki wa Hip Hop, Chemical amefunguka na kueleza jinsi alivyopambana mpaka kufanikisha kushoot video yake ya kwanza ya wimbo Struggling kwa mkopo wa chuo.

Rapper huyo ambaye anafanya poa na video ya wimbo Sielewi ambayo alimshirikisha Soprano Musiq, ameiambia Chilly na Sky kuwa alifanya jitihada zake binafsi ili kufanya kile anachokiamini.
“Baada ya kumaliza kidato cha tano na sita tayari nilikuwa nimesharekodi ngoma nyingi, kwa hiyo nilikuwa na baadhi ya ngoma ambazo nilirekodi. Kuna ngoma ambayo nilipewa offer na Y Cliff jamaa wa EATV, aliniunganisha na Duppy nikafanya ngoma inaitwa ‘Struggling’. Kwa hiyo ile ngoma nilikuwa nayo na ilikuwa ni the best track kwa track zangu zote. So baada ya kuingia chuo kikuu cha Dar es salaam nikasema huu ndio muda wangu wa kufanya mambo yangu yote, nikachukua ile ngoma yangu ‘Struggling’ ili niifanyie kazi. Sasa kipindi hicho muziki tayari ulifika mahali ndio una ngoma lakini hauna video huwezi pewa support, nikasema ngoja mimi nijibane nifanye video, nikaingia location nikafanya video, nakumbuka video yangu ya kwanza niliifanya na boom langu, hela ya chuo,” alisema Chemical
Pia Chemical kwa sasa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment