March 3 2016 Geah Habib kupitia Hekaheka ya Clouds FM leo ametuletea Hekaheka inayomhusu mtoto aliyetolewa kijijini kwa ajili ya kuja kusomeshwa Dar. Tatizo ni pale alipofika Dar na kupewa kazi ya kuuza mboga za majani kutokea Kitunda Dar kuelekea Ubungo Msewe.
‘Alikuja nyumbani akamwambia Mama namuomba mdogo wangu nikaishi naye, Mama akamwambia huyu mtoto anasoma na bila Baba yake siwezi nikamtoa, akasema twende baadae atanisomesha‘>>>Mtoto
‘Tupo na mwingine huko nyumbani ninauza naye mboga na mvulana mwingine yeye kazi yake ni kuhudumia mboga shambani, Tunaamka saa 9 kuja huku kuuza mboga tunapanda kwenye gari na viroba vyetu, wakati mwingine makonda wanatukatalia kupanda, naomba mtusaidie wote na mwenzangu pia anataka kusoma‘>>>Mtoto

0 comments:
Post a Comment