Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam wakati alipotangaza jina la mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka mwaka huu litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambaye ni Mh. Nape Nnauye Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
, amesema Mh. Nape Nnauye amelipa heshima tamasha la pasaka na amethibitisha kuwa mgeni rasmi wa tamasha hilo jijini Mwanza, Msama amemshukuru Waziri Nape kwa kumtambua mungu na kushiriki katika kazi hiyo ya Mungu siku ya tarehe 27 mwezi Machi mwaka huu.
Akiongelea waimbaji ambao tayari wamethiitisha kushiriki katika tamasha hilo amewataba baadhi kuwa ni Upendo Nkone, Faustine Munishi, Ephraim Sekereti kutoka Zambia, Rose Muhando Jesca BM , Bony Mwaiteje na wengine wengi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati alipozungumzia maandalizi ya Tamasha la Pasaka leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari wakati alipozungumzia maandalizi ya Tamasha la Pasaka leo jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment