Thursday, March 24, 2016

jide
Lady Jaydee amefunguka na kuweka wazi sababu zilizomfanya kutumia idea ya ‘Naamka Tena’ kama kampeni ya ujio wake mpya.

Akizungumza kwenye kipindi cha Twenzetu cha Times FM, Jaydee alisema kuwa yeye na timu yake walikaa kuzungumza ni jinsi gani watarudi na katika mawazo yote yaliyowekwa kujadiliwa mezani ndipo wakakubaliana kutumia ‘Naamka Tena’.
“Unajua kuamkaa si lazima uwe ulifumba macho, hata kama ulikaa unaweza sema naamka tena, nilikaa kimya kwa muda mrefu sasa tukaamua tu hii ije mara moja ‘naamka tena’ nashukuru msemo ulikuwa mkubwa sana huu,” alisema.

CHANZO na Bongo5.

0 comments:

Post a Comment