Saturday, March 12, 2016


Wananchi wenye hasira Kali wamechoma moto nyumba na gari pamoja na kumpa kichapo kikali mama mwenye nyumba hiyo anaye fahamika kama MAMA MKASI kwa tuhuma za uchawi na kufuga watoto wezi kwenye nyumba yake.


Kabla ya kuchoma moto nyumba hiyo juzi walimkamata kijana wake mama huyo anaye fahamika kama MKASI ambae ni tapeli maarufu jijini mbeya anye daiwa kuwa kiongozi wa vibaka jiji zima na kumuonya juu ya tabia zake.

Hali ikawa mbaya zaidi leo majira ya saa 3 asubuhi walipochukua sheria mkononi  ya kumvamia mama huyo na kisha kuchoma moto nyumba yake pamoja na Gari moja, Jeshi la Polisi na Zima moto walifika lilifika katika eneo la tukio.

0 comments:

Post a Comment