Saturday, March 19, 2016


RAIS John Magufuli amekabidhi gari la kubeba wagonjwa kwa hospitali ya wilaya ya Chalinze, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani na ahadi ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa wananchi.MAGUFULIIIIIIII

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kwa vyombo vya habari ilisema gari hilo la wagonjwa limekabidhiwa kwa niaba ya Rais na Katibu Mkuu, Ikulu, Peter Ilomo kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete jijini Dar es Salaam.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hilo, Ilomo alisema gari hilo limetolewa na Rais kwa hospitali hiyo, ikiwa ni kuitikia wito na utekelezaji wa ilani na ahadi ya CCM iliyotoa wakati wa uchaguzi ya kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wake nchi nzima.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa Ilomo aliwataka viongozi wa jimbo la Chalinze kulitumia gari hilo kwa matumizi yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi wa eneo hilo.

Akipokea gari hilo kwa niaba ya wananchi wa jimbo na wilaya ya Chalinze, Mbunge Ridhiwani Kikwete alimshukuru Rais Magufuli kwa msaada huo na kuahidi kulitumia gari hilo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuongeza kuwa utendaji kazi wa Rais umekuwa ukiungwa mkono na wananchi wa kada mbalimbali na kuwaomba watanzania kuzidi kumuombea kwa Mungu.

0 comments:

Post a Comment